Nimecheka leo nzima nikiskiza Iyanii akirausha hisi hizi za Nairobi. Akasema:
I am happy today, so happy I am happy today, so happy
Ju sisi ni walevi sisi ni walevi
Tunapenda kamnyweso, tunapenda kamnyweso
Sisi ni walevi, sisi ni walevi
Tunapenda kamnyweso, tunapenda kamnyweso
Furaha-IYANII
We wasemaje kicheko hiki? Kweli labda furaha ni ya walevi tu! Nilibandukia mvinyo bei tupu kwenye jiduka lililofunguliwa hapa karibu–eti wamesema wikendi sitajivuta mbali tena kupata heri kabichi? Nimefurahia.
Furaha, ni kuwa na marafiki
Furaha, ni kulewa na marafiki
Furaha, ni kuwa na marafiki
Furaha, ni kulewa na marafiki
Aiiii-ih
Mnanibamba mbaya, ah wote Tiki (Taka)
Tiki (Taka) Tiki (Taka) Tiki (Taka) Tiki (Taka)
Tiki (Taka) Taka, Taka, Taka
Mnanibamba mbaya!
Furaha-IYANII
Siku zimebaki tatu za wikendi kusherehekea siku ya wafanya kazi jumatatu hii basi sasa tutasingizia kidogo tena sisi wafanya kazi. Ha! Hujafurahia kichecko hiki? Siku hii imekupa nini wewe? Imekupa bima ya afya hata? Wacha usinichoshe.
Mi’ sidhani siku hii ni yetu hata. Sijui ni ya nani, lakini mwenyewe mwambie ametuweza. Hapa nadhani ametupa kweli kizuizi kishindo. Tusisahau kufungua macho yetu nawasihi. Kuna bado kazi. Ama we wasemaje? Kuna kazi kweli.
Mvinyo umekita sukari. Nilisahau nilipo kweli he! Wacha nirudi kwa yule mama pale kidogo. Lazima atakua na my usual. Basi tulewe tusherehekee siku hii ama? Siku ya wafanya kazi imenichekesha! Nitalewa kidogo tu nina kazi Jumapili. Ah! Ama ni Jumanne? (:
Leave a Reply